Wema awavaa Shilole na Nuh Mziwanda.

Sakata la Wema Sepetu kutakwa kimapenzi na mbongo Fleva Nuh Mziwanda, ambaye ni mpenzi wa Shilole,  limeendelea kushika kasi ambapo Wema ameibuka na kuwavua nguo kwa kuwatolea maneno ya shombo. Wema alitoa maneno hayo hivi karibuni baada ya Shilole na Nuh kumgeuka na kusema kwamba alicheza mchezo mchafu ili kuwagombanisha kwa sababu anawaona wanapendana hivyo alimtafuta mtu ambaye anaendana na sauti ya Nuh ili tu amharibie.

Kutokana na maneno hayo Wema alicharuka na kusema kwamba hawezi kutoa rekodi ya uongo na kumsingizia Nuh kwani ni mpuuzi na hawezi kujilinganisha naye kutokana na kwamba ni staa mkubwa.

“Nuh alinipigia na kunitaka kimapenzi ndipo nikaamua kumrekodi na hiyo ni sauti yake haijatengenezwa kama wanavyodai. Kwanza Nuh na Shilole siyo wa kiwango changu, hao ni wasanii wachanga sana, mimi ni staa mkubwa Tanzania na hakuna wa kulinganishwa na mimi labda nje ya Bongo. Naona ni bora nitengeneze kiki kwa kina Davido na wasanii wengine wakubwa duniani, hao si levo yangu jamani,” alisema Wema.

Kabla ya kupatana, Nuh na Shilole waligombana hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni baada ya mrembo huyo kupokea sauti hiyo iliyosikika Nuh akimtongoza Wema.


Leave a comment